Daniel 11:4 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, wakati wa kilele cha uwezo wake, ufalme wake utavunjika na kugawanyika katika sehemu nne kuelekea pepo nne za mbingu. Wazawa wake hawatatawala, wala ufalme hautakuwa mikononi mwa milki aliyotawala, kwa sababu ufalme wake utachukuliwa na wengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kujitokeza, himaya yake itavunjwa na kugawanyika katika pande nne za mbinguni. Hautaenda kwa wazao wake, wala hautakuwa na nguvu alizokuwa nazo, kwa sababu himaya yake itang’olewa na kupewa wengine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atakaposimama, ufalme wake utavunjika, na kugawanyika katika pepo nne za mbinguni; lakini hautakuwa wa uzao wake, wala hautakuwa kama mamlaka yake ambayo alitawala kwayo; kwa maana ufalme wake utang'olewa, hata kwa ajili ya wengine zaidi ya hao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, wakati wa kilele cha uwezo wake, ufalme wake utavunjika na kugawanyika katika sehemu nne kuelekea pepo nne za mbingu. Wazawa wake hawatatawala, wala ufalme hautakuwa mikononi mwa milki aliyotawala, kwa sababu ufalme wake utachukuliwa na wengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kujitokeza, milki yake itavunjwa na kugawanyika katika pande nne za mbinguni. Hautakwenda kwa wazao wake, wala hautakuwa na nguvu alizoonyesha, kwa sababu milki yake itang'olewa na kupewa wengine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kujitokeza, milki yake itavunjwa na kugawanyika katika pande nne za mbinguni. Hautakwenda kwa wazao wake, wala hautakuwa na nguvu alizotumia, kwa sababu milki yake itang’olewa na kupewa wengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hapo, atakapokwisha kuondokea, ufalme wake utavunjika, ukatwe vipande kwenye pepo zote nne za mbinguni; lakini hautakuwa wao walio uzao wake, wala hapatakuwa atakayetawala, kama yeye alivyotawala, kwani ufalme wake utang'olewa, uwe wa wengine, wale wasiupate.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atakaposimama, ufalme wake utavunjika, na kugawanyika katika pepo nne za mbinguni; lakini hautakuwa wa uzao wake, wala hautakuwa kama mamlaka yake ambayo alitawala kwayo; kwa maana ufalme wake utang’olewa, hata kwa ajili ya wengine zaidi ya hao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata hivyo, wakati atakapokuwa na nguvu, ufalme wake utavunjika na kugawanyika katika sehemu ine kuelekea pande ine za mbingu. Wazao wake hawatatawala, wala ufalme hautakuwa katika mikono ya urizi aliotawala, kwa sababu ufalme wake utakamatwa na wengine.