Daniel 11:40 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Wakati wa mwisho mfalme wa kusini atamshambulia mfalme huyo wa kaskazini. Lakini mfalme wa kaskazini atajibu mashambulio hayo kwa nguvu kama kimbunga, akitumia magari ya farasi, wapandafarasi na meli nyingi. Atazivamia nchi nyingi na kupita katika nchi hizo kama mafuriko ya maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Wakati wa mwisho, mfalme wa Kusini atapigana naye vita, naye mfalme wa Kaskazini atamshambulia kwa magari ya vita, askari wapanda farasi, na idadi kubwa ya meli. Atavamia nchi nyingi na kuzikumba nchi hizo kama mafuriko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Wakati wa mwisho mfalme wa kusini atamshambulia mfalme huyo wa kaskazini. Lakini mfalme wa kaskazini atajibu mashambulio hayo kwa nguvu kama kimbunga, akitumia magari ya farasi, wapandafarasi na meli nyingi. Atazivamia nchi nyingi na kupita katika nchi hizo kama mafuriko ya maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Katika wakati wa mwisho mfalme wa Kusini atapigana naye vita, naye mfalme wa Kaskazini atamshambulia kwa magari ya vita na askari wapanda farasi na idadi kubwa ya meli. Atavamia nchi nyingi na kukumba nchi hizo kama mafuriko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Katika wakati wa mwisho, mfalme wa Kusini atapigana naye vita, naye mfalme wa Kaskazini atamshambulia kwa magari ya vita, askari wapanda farasi, na idadi kubwa ya meli. Atavamia nchi nyingi na kuzikumba nchi hizo kama mafuriko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku za mwisho mfalme wa kusini atapigana naye; ndipo, naye mfalme wa kaskazini atakapomkimbilia kama upepo wa kimbunga kwa magari pamoja na wapanda farasi na kwa merikebu nyingi, aziingie hizo nchi na kuzifurikia na kuzieneza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa mwisho mufalme wa kusini atamushambulia mufalme huyo wa kaskazini. Lakini mufalme wa kaskazini atajibu mashambulio hayo kwa nguvu kama zoruba, akitumia magari ya vita, waaskari wapanda-farasi na mashua nyingi. Atashambulia inchi nyingi na kupita katika inchi hizo kama mafuriko ya maji.