Daniel 11:43 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na vito vyote vya thamani vya nchi ya Misri. Watu wa Libia na watu wa Kushi watafuata nyayo zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atamiliki hazina za dhahabu na fedha na utajiri wote wa Misri, huku Walibia na Wakushi wakijisalimisha kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na vito vyote vya thamani vya nchi ya Misri. Watu wa Libia na watu wa Kushi watafuata nyayo zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na utajiri wote wa Misri, pamoja na Walibya na Wakushi kwa kujisalimisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na utajiri wote wa Misri, pamoja na Walibia na Wakushi kwa kujisalimisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo mikononi mwake mwenye nguvu vitakuwamo vilimbiko vya dhahabu na vya fedha na vyombo vyote vya Misri vipendezavyo; kwa hiyo nao Walibia na Wanubi watamfuata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atatwaa akiba za zahabu, feza na mawe yote ya bei kali ya inchi ya Misri. Watu wa Libya na watu wa Etiopia watamufuata.