Daniel 11:45 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo, atapiga mahema yake makubwa kati ya bahari na mlima mtukufu na mtakatifu. Lakini atakuwa amefikia kikomo chake, na hatakuwapo yeyote wa kumsaidia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atasimika mahema yake ya ufalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa kupendeza. Hata hivyo, atafikia mwisho wake, wala hakuna yeyote atakayemsaidia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo, atapiga mahema yake makubwa kati ya bahari na mlima mtukufu na mtakatifu. Lakini atakuwa amefikia kikomo chake, na hatakuwapo yeyote wa kumsaidia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atasimika mahema yake ya kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa kupendeza. Hata hivyo, atafikia mwisho wake, wala hakuna ye yote atakayemsaidia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atasimika hema zake za ufalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa kupendeza. Hata hivyo, atafikia mwisho wake, wala hakuna yeyote atakayemsaidia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Atalipiga hema lake la kifalme katikati ya bahari na ya mlima wenye utukufu na utakatifu; ndipo, mwisho wake utakapokuja, lakini hatakuwako atakayemsaidia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaidi ya hayo, atapiga mahema yake makubwa kati ya bahari na mulima mutukufu na mutakatifu. Lakini atakuwa amefikia ukomo wake, na hakutakuwa mutu yeyote wa kumusaidia.