Daniel 11:5 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Mfalme wa kusini atakuwa mwenye nguvu. Lakini mmoja wa majemadari wake atakuwa na nguvu kuliko yeye na utawala wake utakuwa mkubwa zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu, lakini mmoja wa majemadari wake atakuwa na nguvu zaidi yake, naye atatawala ufalme wake mwenyewe kwa nguvu nyingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mfalme wa kusini atakuwa hodari; na mmoja wa wakuu wake atakuwa hodari kuliko yeye, naye atakuwa na mamlaka; mamlaka yake itakuwa mamlaka kubwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Mfalme wa kusini atakuwa mwenye nguvu. Lakini mmoja wa majemadari wake atakuwa na nguvu kuliko yeye na utawala wake utakuwa mkubwa zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu, lakini mmoja wa majemadari wake atakuwa na nguvu zaidi kuliko mfalme, naye atatawala ufalme wake mwenyewe kwa nguvu nyingi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu, lakini mmoja wa majemadari wake atakuwa na nguvu zaidi kuliko mfalme, naye atatawala ufalme wake mwenyewe kwa nguvu nyingi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme wa kusini atapata nguvu, lakini mmoja wa wakuu wake atapata nguvu kumshinda mwenyewe, kisha atatawala kwa uwezo, nao ufalme wake utakuwa mkubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mfalme wa kusini atakuwa hodari; na mmoja wa wakuu wake atakuwa hodari kuliko yeye, naye atakuwa na mamlaka; mamlaka yake itakuwa mamlaka kubwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme wa kusini atakuwa mwenye nguvu. Lakini mumoja wa majemadari wake atakuwa na nguvu kuliko yeye na utawala wake utakuwa mukubwa zaidi.