Daniel 11:6 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya miaka kadhaa, watafanya mkataba; binti mfalme wa kusini ataolewa katika jamaa ya mfalme na kuratibisha huo mkataba; wa kaskazini, lakini hataendelea kuwa na nguvu, pia mfalme na wazawa wake hawatavumilia; na huyo binti, mwanawe na watumwa wa kike aliokwenda nao, wote watauawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya miaka kadhaa, wataungana. Binti ya mfalme wa Kusini ataolewa kwa mfalme wa Kaskazini ili kuimarisha mapatano, lakini nguvu za huyo binti hazitadumu; hata mfalme hatadumu wala nguvu zake. Katika siku hizo atafukuzwa, pamoja na hao wasindikizaji wake wa kifalme, na baba yake, na yeyote aliyemuunga mkono.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baada ya miaka kadha wa kadha watashirikiana; kwa kuwa binti wa mfalme wa kusini atakuja kwa mfalme wa kaskazini, ili kufanya mapatano naye; lakini hatakuwa na nguvu za mkono wake sikuzote; wala mfalme yule hatasimama, wala mkono wake; lakini yule binti atatolewa, na hao waliomleta, na yeye aliyemzaa, na yeye aliyemtia nguvu, zamani zile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya miaka kadhaa, watafanya mkataba; binti mfalme wa kusini ataolewa katika jamaa ya mfalme na kuratibisha huo mkataba; wa kaskazini, lakini hataendelea kuwa na nguvu, pia mfalme na wazawa wake hawatavumilia; na huyo binti, mwanawe na watumwa wa kike aliokwenda nao, wote watauawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya miaka kadha wa kadha, wataungana. Binti wa mfalme wa Kusini ataolewa kwa mfalme wa Kaskazini ili kuimarisha mapatano, lakini huyo binti nguvu zake za ushawishi hazitadumu, vivyo hivyo na baba yake. Katika siku hizo atafukuzwa, pamoja na hao wasindikizaji wake wa kifalme, watoto wake na ye yote aliyemuunga mkono.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya miaka kadha, wataungana. Binti wa mfalme wa Kusini ataolewa kwa mfalme wa Kaskazini ili kuimarisha mapatano, lakini huyo binti nguvu zake hazitadumu; hata mfalme hatadumu wala nguvu zake. Katika siku hizo atafukuzwa, pamoja na hao wasindikizaji wake wa kifalme, watoto wake, na yeyote aliyemuunga mkono.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miaka itakapopita, watafanya mapatano, naye binti mfalme wa kusini atakwenda kwake mfalme wa kaskazini kutengeneza matengenezo, lakini naye yule binti mfalme nguvu za mkono wake zitampotea, yule mfalme asikae na nguvu za mkono; ndipo, yule binti mfalme atakapotolewa pamoja nao waliompeleka na mzazi wake naye aliyemtia nguvu siku zile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baada ya miaka kadha wa kadha watashirikiana; kwa kuwa binti wa mfalme wa kusini atakuja kwa mfalme wa kaskazini, ili kufanya mapatano naye; lakini hatakuwa na nguvu za mkono wake sikuzote; wala mfalme yule hatasimama, wala mkono wake; lakini yule binti atatolewa, na hao waliomleta, na yeye aliyemzaa, na yeye aliyemtia nguvu, zamani zile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha miaka michache, wataungana pamoja; binti wa mufalme wa kusini ataolewa katika jamaa ya mufalme wa kaskazini na kutimiza mapatano hayo, lakini hataendelea kuwa na nguvu, hata mufalme na wazao wake hawatavumilia; na huyo binti, mwana wake na wajakazi aliokwenda nao, wote watauawa.