Daniel 11:8 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atazibeba sanamu za kusubu za miungu yao na vyombo vya thamani vya fedha na dhahabu mpaka nchini Misri. Kwa muda wa miaka kadhaa, mfalme wa kusini hatamshambulia mfalme wa kaskazini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tena ataitwaa miungu yao, vinyago vyao vya chuma, na vitu vyao vya thamani vya fedha na dhahabu, na kuvichukua hadi Misri. Kwa miaka kadhaa atamwacha mfalme wa Kaskazini bila kumsumbua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na miungu yao, pamoja na sanamu zao, na vyombo vyao vizuri vya fedha na dhahabu atavichukua mpaka Misri; kisha atajizuia miaka kadha wa kadha asimwendee mfalme wa kaskazini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atazibeba sanamu za kusubu za miungu yao na vyombo vya thamani vya fedha na dhahabu mpaka nchini Misri. Kwa muda wa miaka kadhaa, mfalme wa kusini hatamshambulia mfalme wa kaskazini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye ataitwaa miungu yao, vinyago vyao vya chuma na vitu vyao vya thamani vya fedha na dhahabu na kuvichukua hadi Misri kama nyara za vita. Kwa miaka kadha wa kadha atamwacha mfalme wa Kaskazini bila kumsumbua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tena ataitwaa miungu yao, vinyago vyao vya chuma, na vitu vyao vya thamani vya fedha na dhahabu, na kuvichukua hadi Misri. Kwa miaka kadha atamwacha mfalme wa Kaskazini bila kumsumbua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, atakapoichukua miungu yao na vinyago vyao na vyombo vyao viwapendezavyo vya fedha na vya dhahabu, ataviteka na kuvipeleka Misri, kisha atakaa miaka na miaka, asimwendee tena mfalme wa kaskazini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na miungu yao, pamoja na sanamu zao, na vyombo vyao vizuri vya fedha na dhahabu atavichukua mpaka Misri; kisha atajizuia miaka kadha wa kadha asimwendee mfalme wa kaskazini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atabeba sanamu za miungu yao na vyombo vya bei kali vya feza na zahabu mpaka katika inchi ya Misri. Kwa muda wa miaka michache, mufalme wa kusini hatamushambulia mufalme wa kaskazini.