Daniel 12:11 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Tangu wakati wa kukomeshwa kwa sadaka za kuteketezwa kila siku, yaani kutoka wakati ule chukizo haribifu litakaposimamishwa itakuwa muda wa siku 1,290.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tangu wakati ule wa kukomeshwa kwa dhabihu ya kila siku, na kuanzishwa kwa chukizo la uharibifu, kutakuwepo siku elfu moja na mia mbili na tisini (1,290).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Tangu wakati wa kukomeshwa kwa sadaka za kuteketezwa kila siku, yaani kutoka wakati ule chukizo haribifu litakaposimamishwa itakuwa muda wa siku 1,290.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tangu wakati ule wa kukomeshwa dhabihu ya kila siku na kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu kutakuweko siku 1,290.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tangu wakati ule wa kukomeshwa dhabihu ya kila siku na kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu, kutakuwako siku 1,290.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tangu hapo, matambiko ya kila siku yatakapoondolewa, mahali pao pawekwe mwangamizaji atapishaye, ni siku 1290.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tangu wakati wa kukomeshwa kwa sadaka za kuteketezwa kwa moto za kila siku, ni kusema kutoka wakati ule chukizo linaloleta uharibifu litakaposimamishwa, itakuwa muda wa siku elfu moja mia mbili na makumi kenda.