Daniel 12:4 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ila sasa, Danieli, weka siri mambo hayo; kifunge kitabu na kukitia mhuri mpaka wakati wa mwisho utakapofika. Wengi watakimbilia huko na huko, na maarifa yataongezeka.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wewe Danieli, yafunge na kuyatia muhuri maneno ya kitabu hiki hadi wakati wa mwisho. Wengi wataenda hapa na pale, na maarifa yataongezeka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ila sasa, Danieli, weka siri mambo hayo; kifunge kitabu na kukitia mhuri mpaka wakati wa mwisho utakapofika. Wengi watakimbilia huko na huko, na maarifa yataongezeka.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wewe Danieli, yafunge na kuyatia muhuri maneno ya kitabu hiki mpaka wakati wa mwisho. Wengi watakwenda huku na huko na maarifa yataongezeka.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wewe Danieli, yafunge na kuyatia muhuri maneno ya kitabu hiki mpaka wakati wa mwisho. Wengi watakwenda huku na huko, na maarifa yataongezeka.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe wewe Danieli, yafunge haya maneno, nacho kitabu kitie muhuri, mpaka siku za mwisho zitakapotimia! Ndipo, wengi watakapokichunguza, utambuzi wao uongezeke.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa, Danieli, weka kwa siri mambo hayo; funga kitabu na kutia muhuri juu yake mpaka wakati wa mwisho utakapofika. Wengi watakimbilia huko na huko, na maarifa yataongezeka.