Daniel 2:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale Wakaldayo wakamjibu: “Mfalme, hakuna mtu yeyote duniani awezaye kutimiza matakwa yako. Hakuna mfalme yeyote, hata awe mkuu na mwenye nguvu kiasi gani aliyepata kuwauliza waganga au walozi au Wakaldayo jambo kama hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanajimu wakamjibu mfalme, “Hakuna mtu duniani ambaye anaweza kufanya analotaka mfalme! Vilevile, hakuna mfalme, hata awe mkuu na mwenye uweza namna gani, aliyeuliza kitu kama hicho kwa mganga, au kwa msihiri, wala kwa mnajimu yeyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme, wakasema, Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme; kwa maana hapana mfalme, wala bwana, wala liwali, aliyetaka neno kama hili kwa mganga, wala kwa mchawi, wala kwa Mkaldayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale Wakaldayo wakamjibu: “Mfalme, hakuna mtu yeyote duniani awezaye kutimiza matakwa yako. Hakuna mfalme yeyote, hata awe mkuu na mwenye nguvu kiasi gani aliyepata kuwauliza waganga au walozi au Wakaldayo jambo kama hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanajimu wakamjibu mfalme, “Hakuna mtu duniani ambaye anaweza kufanya analotaka mfalme! Vile vile hakuna mfalme hata awe mkuu na mwenye uweza namna gani, aliyeuliza kitu kama hicho kwa mganga au kwa msihiri, wala kwa mnajimu ye yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanajimu wakamjibu mfalme, “Hakuna mtu duniani ambaye anaweza kufanya analotaka mfalme! Vilevile hakuna mfalme hata awe mkuu na mwenye uweza namna gani, aliyeuliza kitu kama hicho kwa mganga au kwa msihiri, wala kwa mnajimu yeyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakasidi wakamjibu mfalme kwamba: Hakuna mtu ulimwenguni anayeweza kulieleza hilo neno la mfalme; kwani hakuna mfalme ye yote, ingawa ni mkuu mwenye nguvu, aliyetaka jambo kama hilo kwao wote walio waandishi na waaguaji na Wakasidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme, wakasema, Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme; kwa maana hapana mfalme, wala bwana, wala liwali, aliyetaka neno kama hili kwa mganga, wala kwa mchawi, wala kwa Mkaldayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale Wakaldea wakamujibu: Mufalme, hakuna mutu yeyote katika dunia anayeweza kutimiza mapenzi yako. Hakuna mufalme yeyote, hata akuwe mukubwa na mwenye nguvu yapata gani aliyepata kuwauliza waganga au walozi au Wakaldea jambo kama hilo.