Daniel 2:15 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akamwuliza, “Kwa nini amri ya mfalme ni kali hivyo?” Hapo Arioko akamsimulia Danieli kisa chote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamuuliza huyo afisa wa mfalme, “Kwa nini mfalme ametoa amri kali hivyo?” Ndipo Arioko akamweleza Danieli jambo hilo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
alijibu, akamwambia Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, Mbona amri hii ya mfalme ina ukali namna hii? Ndipo Arioko akamwarifu Danieli habari ile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akamwuliza, “Kwa nini amri ya mfalme ni kali hivyo?” Hapo Arioko akamsimulia Danieli kisa chote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwuliza huyo afisa wa mfalme, “Kwa nini mfalme ametoa amri kali hivyo?” Ndipo Arioko akamweleza Danieli jambo hilo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamuuliza huyo afisa wa mfalme, “Kwa nini mfalme ametoa amri kali hivyo?” Ndipo Arioko akamweleza Danieli jambo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, akamwuliza Arioki, kwa kuwa ni mtu wa nguvu wa mfalme: Mbona amri hiyo kali imetoka kwake mfalme? Arioki alipomjulisha Danieli jambo hilo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
alijibu, akamwambia Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, Mbona amri hii ya mfalme ina ukali namna hii? Ndipo Arioko akamwarifu Danieli habari ile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Danieli akamwuliza: Kwa nini amri ya mufalme ni kali hivyo? Arioki akamwelezea Danieli maneno yote.