Daniel 2:16 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Danieli alipomwendea mfalme na kumwomba ampe muda ili aweze kumjulisha mfalme maana ya ndoto yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Danieli akawaendea mfalme, akamwomba ampe muda ili aweze kumfasiria ile ndoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Danieli alipomwendea mfalme na kumwomba ampe muda ili aweze kumjulisha mfalme maana ya ndoto yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika jambo hili, Danieli akamwendea mfalme akamwomba ampe muda, ili aweze kumfasiria ile ndoto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliposikia jambo hili, Danieli akamwendea mfalme, akamwomba ampe muda ili aweze kumfasiria ile ndoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Danieli akaingia kwa mfalme, akamwomba, ampe siku kidogo, apate kumweleza mfalme maana ya ndoto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Danieli alimwendea mufalme na kumwomba amupatie muda kusudi apate kumujulisha mufalme maana ya ndoto yake.