Daniel 2:21 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hubadilisha nyakati na majira, huwaondoa na kuwatawaza wafalme. Wenye busara huwapa hekima, wenye maarifa huwaongezea ufahamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye hubadili nyakati na majira; huwaweka wafalme na kuwaondoa. Huwapa hekima wenye hekima, na maarifa wenye ufahamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hubadilisha nyakati na majira, huwaondoa na kuwatawaza wafalme. Wenye busara huwapa hekima, wenye maarifa huwaongezea ufahamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye hubadili nyakati na majira, huwaweka wafalme na kuwaondoa. Huwapa hekima wenye hekima na maarifa wenye ufahamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye hubadili nyakati na majira; huwaweka wafalme na kuwaondoa. Huwapa hekima wenye hekima, na maarifa wenye ufahamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeye ndiye anayezigeuza siku na miaka, ndiye anayeondoa wafalme, tena ndiye anayeweka wafalme, ndiye anayewapa wajuzi ujuzi, nao watambuzi huwapa utambuzi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Anabadilisha nyakati na wakati, anaondoa na kuwatawalisha wafalme. Anawapa hekima wenye hekima, anawaongezea wenye maarifa ufahamu.