Daniel 2:24 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Danieli akamwendea Arioko aliyekuwa ameteuliwa kuwaangamiza wenye hekima wa Babuloni, akamwambia, “Usiwaue wenye hekima wa Babuloni, ila nipeleke mimi mbele ya mfalme, nami nitamweleza maana ya ndoto yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Danieli akamwendea Arioko, ambaye mfalme alikuwa amemteua kuwaua wenye hekima wa Babeli, akamwambia, “Usiwaue wenye hekima wa Babeli. Nipeleke kwa mfalme, nami nitamfasiria ndoto yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Danieli akaenda kwa Arioko, aliyewekwa na mfalme kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli; alikwenda akamwambia hivi, Usiwaangamize wenye hekima wa Babeli; niingize mimi mbele ya mfalme, nami nitamwonyesha mfalme ile tafsiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Danieli akamwendea Arioko aliyekuwa ameteuliwa kuwaangamiza wenye hekima wa Babuloni, akamwambia, “Usiwaue wenye hekima wa Babuloni, ila nipeleke mimi mbele ya mfalme, nami nitamweleza maana ya ndoto yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Danieli akamwendea Arioko, ambaye mfalme alikuwa amemteua kuwaua wenye hekima wa Babeli, akamwambia, “Usiwaue wenye hekima wa Babeli. Nipeleke kwa mfalme, nami nitamfasiria ndoto yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Danieli akamwendea Arioko, ambaye mfalme alikuwa amemteua kuwaua wenye hekima wa Babeli, akamwambia, “Usiwaue wenye hekima wa Babeli. Nipeleke kwa mfalme, nami nitamfasiria ndoto yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Danieli alipokwenda kwake Arioki, mfalme aliyemwagiza kuwaua wajuzi wa Babeli; alipofika akamwambia: Wajuzi wa Babeli usiwaue! Ila nipeleke kwake mfalme, nimweleze mfalme maana ya ndoto!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Danieli akaenda kwa Arioko, aliyewekwa na mfalme kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli; alikwenda akamwambia hivi, Usiwaangamize wenye hekima wa Babeli; niingize mimi mbele ya mfalme, nami nitamwonyesha mfalme ile tafsiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Danieli akamwendea Arioki aliyekuwa amechaguliwa kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli, akamwambia: Usiwaue wenye hekima wa Babeli, lakini unipeleke mimi mbele ya mufalme, nami nitamweleza maana ya ndoto yake.