Daniel 2:28 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, yuko Mungu mbinguni ambaye hufumbua mafumbo, naye amekujulisha, ee mfalme Nebukadneza, mambo yatakayotukia siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyokujia kichwani mwako ulipokuwa umelala ni haya:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Amemwonesha Mfalme Nebukadneza kitakachotokea siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyopita mawazoni mwako ulipokuwa umelala kitandani mwako ni haya:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, yuko Mungu mbinguni ambaye hufumbua mafumbo, naye amekujulisha, ee mfalme Nebukadneza, mambo yatakayotukia siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyokujia kichwani mwako ulipokuwa umelala ni haya:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Amemwonyesha Mfalme Nebukadneza kitakachotokea siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyopita akilini mwako ulipokuwa umelala kitandani mwako ni haya:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Amemwonyesha Mfalme Nebukadneza kitakachotokea siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyopita mawazoni mwako ulipokuwa umelala kitandani mwako ni haya:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini juu mbinguni yuko Mungu anayefunua mafumbo: yeye anamjulisha mfalme Nebukadinesari yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako na maono yaliyokuwa mbele yako, ulipolala kitandani, ndiyo haya:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, kuna Mungu mbinguni ambaye anafumbua mafumbo, naye amekujulisha, ee mufalme Nebukadneza, mambo yatakayotukia katika siku zinazokuja. Ndoto yako na maono yaliyokufikia ulipokuwa unalala ni haya: