Daniel 2:29 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwako ee mfalme, ulipokuwa umelala kitandani mwako, yalikujia mawazo kuhusu mambo yatakayotukia baadaye; naye Mungu afumbuaye mafumbo, alikuonesha yale yatakayotukia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ee mfalme, ulipokuwa umelala kitandani, yalikujia mawazo kuhusu mambo yatakayotokea baadaye, naye mfunuaji wa siri akakuonesha ni kitu gani kitakachotokea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwako ee mfalme, ulipokuwa umelala kitandani mwako, yalikujia mawazo kuhusu mambo yatakayotukia baadaye; naye Mungu afumbuaye mafumbo, alikuonesha yale yatakayotukia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ee mfalme, ulipokuwa umelala kitandani, yalikujia mawazo kuhusu mambo yatakayotokea baadaye, naye mfunuaji wa siri akakuonyesha ni kitu gani kitakachotokea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ee mfalme, ulipokuwa umelala kitandani, yalikujia mawazo kuhusu mambo yatakayotokea baadaye, naye mfunuaji wa siri akakuonyesha ni kitu gani kitakachotokea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe mfalme ulipolala kitandani, yakakuinukia mawazo ya mambo yatakayokuwa halafu; ndipo, yeye afunuaye mafumbo alipokujulisha yatakayokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee mufalme, ulipokuwa unalala katika kitanda chako, mawazo yalikufikia juu ya mambo yatakayotukia kisha; naye Mungu anayefumbua mafumbo, alikuonyesha yale yatakayotukia.