Daniel 2:30 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mimi sikufumbuliwa fumbo hili kwa sababu nina hekima kuliko wanaadamu wengine, bali ili wewe mfalme, upate kujulishwa maana ya ndoto yako na kujua mawazo yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwangu mimi, nimefunuliwa siri hii, si kwa sababu nina hekima kubwa kuliko watu wengine wanaoishi, bali ili wewe, ee mfalme, upate kujua tafsiri, na ili uweze kuelewa kile kilichopita mawazoni mwako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mimi sikufumbuliwa fumbo hili kwa sababu nina hekima kuliko wanaadamu wengine, bali ili wewe mfalme, upate kujulishwa maana ya ndoto yako na kujua mawazo yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwangu mimi, siri hii imefunuliwa kwangu, si kwa sababu nina hekima kubwa kuliko watu wengine wanaoishi, bali ni ili wewe, Ee mfalme, upate kujua tafsiri na ili uweze kuelewa kile kilichopita akilini mwako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwangu mimi, nimefunuliwa siri hii, si kwa sababu nina hekima kubwa kuliko watu wengine wanaoishi, bali ni ili wewe, ee mfalme, upate kujua tafsiri, na ili uweze kuelewa kile kilichopita mawazoni mwako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nami sikufunuliwa fumbo hilo kwa kwamba ninao ujuzi kuliko wengine walipo, ila ni kwa kwamba mfalme ajulishwe maana ya ndoto, upate kuyajua, uliyoyawaza moyoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mimi sikufumbuliwa fumbo hili kwa sababu nina hekima kuliko wanadamu wengine, lakini kusudi wewe mufalme, upate kujulishwa maana ya ndoto yako na kujua mawazo yako.