Daniel 2:31 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Katika ndoto yako, ee mfalme, uliona sanamu kubwa, yenye nguvu na iliyongaa sana, imesimama mbele yako. Sanamu hiyo ilikuwa ya kutisha mno.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ee mfalme, ulitazama, na mbele yako ilisimama sanamu kubwa mno, iliyong’aa kupita kiasi na yenye kutisha kwa mwonekano wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Katika ndoto yako, ee mfalme, uliona sanamu kubwa, yenye nguvu na iliyong'aa sana, imesimama mbele yako. Sanamu hiyo ilikuwa ya kutisha mno.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ee mfalme, ulitazama na mbele yako ilisimama sanamu kubwa, kubwa mno kupita kiasi, sanamu inayong'aa inayotisha kwa kuonekana kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ee mfalme, ulitazama, na mbele yako ilisimama sanamu kubwa, kubwa mno kupita kiasi, sanamu iliyong’aa na kutisha kwa kuonekana kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe mfalme ulikuwa ukiota, mara ukaona kinyago kimoja. Kinyago hicho kilikuwa kikubwa sana, kikametuka kabisa, kikasimama mbele yako, kikatia woga kwa kutazamwa tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika ndoto yako, ee mufalme, uliona sanamu kubwa, yenye nguvu na iliyoangaa sana, ikisimama mbele yako. Sanamu hiyo ilikuwa ya kutisha sana.