Daniel 2:34 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukiwa bado unaangalia, jiwe lilingoka lenyewe, bila kuguswa, na kuipondaponda miguu ya shaba na udongo wa mfinyanzi ya ile sanamu, na kuivunja vipandevipande.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo, na kuivunja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukiwa bado unaangalia, jiwe liling'oka lenyewe, bila kuguswa, na kuipondaponda miguu ya shaba na udongo wa mfinyanzi ya ile sanamu, na kuivunja vipandevipande.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo wa mfinyanzi na kuivunja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo wa mfinyanzi, na kuivunja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ulipokuwa unakitazama, mara jiwe likaporomoka lenyewe lisilotupwa na mikono ya watu, likakipiga kile kinyago penye miguu yake iliyokuwa ya chuma na ya udongo, likaiponda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ulipokuwa ukiangalia, jiwe liliongoka lenyewe, bila kuguswa, na kuipondaponda miguu ya shaba na udongo wa mufinyanzi ya ile sanamu, na kuivunja vipandevipande.