Daniel 2:38 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amekupa mamlaka juu ya wanaadamu wote, wanyama wa porini na ndege wote wa angani, kokote kule waliko. Wewe ndiwe kile kichwa cha dhahabu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mikononi mwako amewaweka wanadamu, wanyama wa kondeni, na ndege wa angani. Popote wanapoishi, amekufanya wewe kuwa mtawala wa hao wote. Wewe ndiwe kile kichwa cha dhahabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amekupa mamlaka juu ya wanaadamu wote, wanyama wa porini na ndege wote wa angani, kokote kule waliko. Wewe ndiwe kile kichwa cha dhahabu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mikononi mwako amewaweka wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani. Po pote waishipo amekufanya wewe kuwa mtawala juu yao wote. Wewe ndiye kile kichwa cha dhahabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mikononi mwako amewaweka wanadamu, wanyama wa kondeni, na ndege wa angani. Popote waishipo amekufanya wewe kuwa mtawala juu yao wote. Wewe ndiye kile kichwa cha dhahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pote panapokaa watu na nyama wa porini na ndege wa angani amepatia mkononi mwako, uwatawale hao wote. Wewe ndiwe kichwa cha dhahabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amekupa mamlaka juu ya wanadamu wote, nyama wa pori na ndege wote, popote kule wanapokuwa. Wewe ndiwe kile kichwa cha zahabu!