Daniel 2:39 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada yako utafuata ufalme mwingine, lakini ufalme huo utakuwa dhaifu. Huu utafuatwa na ufalme wa tatu unaofananishwa na shaba; huo utaitawala dunia yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Baada yako, ufalme mwingine utainuka, ulio dhaifu kuliko wako. Baadaye utafuata ufalme wa tatu, ule wa shaba, nao utaitawala dunia yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada yako utafuata ufalme mwingine, lakini ufalme huo utakuwa dhaifu. Huu utafuatwa na ufalme wa tatu unaofananishwa na shaba; huo utaitawala dunia yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Baada yako, ufalme mwingine utainuka, ulio dhaifu kuliko wako. Baadaye, utafuata ufalme wa tatu, ule wa shaba, utatawala juu ya dunia yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Baada yako, ufalme mwingine utainuka, ulio dhaifu kuliko wako. Baadaye utafuata ufalme wa tatu, ule wa shaba, nao utatawala juu ya dunia yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyuma yako utatokea ufalme mwingine usio na nguvu kama wako. Kisha utafuata ufalme wa tatu, ni wa shaba utazitawala nchi zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma yako kutafuata ufalme mwingine, lakini ufalme huo utakuwa zaifu. Huu utafuatwa na ufalme wa tatu unaofananishwa na shaba; huo utaitawala dunia yote.