Daniel 2:40 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya falme hizo, utafuata ufalme mwingine imara kama chuma. Na kama vile chuma kivunjavyo na kupondaponda vitu vyote, ndivyo ufalme huo utakavyovunjavunja na kusagilia mbali falme zilizotangulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hatimaye kutakuwako na ufalme wa nne, wenye nguvu kama chuma, kwa maana chuma huvunja na kupondaponda kila kitu; kama vile chuma ivunjavyo vitu vipande vipande, ndivyo ufalme huo utakavyopondaponda na kuvunjavunja nyingine zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya falme hizo, utafuata ufalme mwingine imara kama chuma. Na kama vile chuma kivunjavyo na kupondaponda vitu vyote, ndivyo ufalme huo utakavyovunjavunja na kusagilia mbali falme zilizotangulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hatimaye, kutakuweko na ufalme wa nne, wenye nguvu kama chuma, kwa maana chuma huvunja na kupondaponda kila kitu, kama vile chuma ivunjavyo vitu vipande vipande, ndivyo ufalme huo utakavyopondaponda na kuvunjavunja nyingine zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hatimaye, kutakuwako na ufalme wa nne, wenye nguvu kama chuma, kwa maana chuma huvunja na kupondaponda kila kitu; kama vile chuma ivunjavyo vitu vipande vipande, ndivyo ufalme huo utakavyopondaponda na kuvunjavunja nyingine zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha utakuwa ufalme wa nne wenye nguvu kama za chuma; kama chuma kinavyovunja na kuponda vyote kabisa, ndivyo, utakavyoponda na kuuvunja ufalme wote mwingine kama chuma chenye kuvunja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya falme hizo, kutafuata ufalme mwingine wenye kuwa imara kama chuma. Na kama vile chuma kinavyovunja na kupondaponda vitu vyote, ndivyo ufalme huo utakavyovunjavunja na kusaga kabisa falme zilizotangulia.