Daniel 2:41 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uliona pia kuwa nyayo na vidole vya sanamu hiyo vilikuwa nusu udongo wa mfinyanzi na nusu chuma. Hii ina maana kwamba ufalme huo utagawanyika; lakini utakuwa na kiasi fulani cha nguvu za chuma kwa sababu kulikuwa na chuma kilichochanganyikana na udongo wa mfinyanzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama ulivyoona nyayo na vidole, sehemu moja vikiwa vya udongo uliochomwa na sehemu nyingine vya chuma, kadhalika ufalme huu utakuwa umegawanyika; hata hivyo, utakuwa wenye nguvu ya chuma ndani yake kama ulivyoona chuma kikiwa kimechanganywa na udongo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uliona pia kuwa nyayo na vidole vya sanamu hiyo vilikuwa nusu udongo wa mfinyanzi na nusu chuma. Hii ina maana kwamba ufalme huo utagawanyika; lakini utakuwa na kiasi fulani cha nguvu za chuma kwa sababu kulikuwa na chuma kilichochanganyikana na udongo wa mfinyanzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile ulivyoona kuwa kwa sehemu nyayo na vidole vilikuwa vya udongo wa mfinyanzi uliochomwa na kwa sehemu nyingine chuma, hivyo huu utakuwa ufalme uliogawanyikagawanyika, hata hivyo kutakuwa na baadhi zenye nguvu za chuma ndani yake, kama vile ulivyoona chuma imechanganywa na udongo wa mfinyanzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile ulivyoona kuwa kwa sehemu nyayo na vidole vilikuwa vya udongo wa mfinyanzi uliochomwa na kwa sehemu nyingine chuma, hivyo huu utakuwa ufalme uliogawanyika; hata hivyo utakuwa na sehemu zenye nguvu za chuma ndani yake, kama vile ulivyoona chuma imechanganywa na udongo wa mfinyanzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hivyo, ulivyoiona miguu yake na vidole vyake kuwa nusu yao ya udongo na nusu yao ya chuma, utakuwa ufalme uliogawanyika: upande utakuwa wenye nguvu za chuma, sawasawa kama ulivyoona chuma kilichochanganyika na udongo wa mfinyanzi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uliona vilevile kwamba vikanyagio na vidole vya sanamu hiyo vilikuwa nusu udongo wa mufinyanzi na nusu chuma. Hii ina maana kwamba ufalme huo utagawanyika; lakini ndani yake kutakuwa nguvu za chuma kwa sababu kulikuwa chuma kilichochanganyikana na udongo wa mufinyanzi.