Daniel 2:42 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama ulivyoona, vidole vyake vya miguu vilikuwa nusu chuma na nusu udongo wa mfinyanzi, na hii inamaanisha kwamba ufalme huo utakuwa na nguvu kiasi fulani na udhaifu kiasi fulani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile vidole vyake vya miguu vilikuwa kwa sehemu chuma na kwa sehemu udongo, ndivyo ufalme huo kwa sehemu utakuwa na nguvu na kwa sehemu udhaifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama ulivyoona, vidole vyake vya miguu vilikuwa nusu chuma na nusu udongo wa mfinyanzi, na hii inamaanisha kwamba ufalme huo utakuwa na nguvu kiasi fulani na udhaifu kiasi fulani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile vidole vyake vya miguu vilikuwa kwa sehemu chuma na sehemu udongo wa mfinyanzi, hivyo ufalme huo kwa sehemu utakuwa na nguvu na kwa sehemu udhaifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile vidole vyake vya miguu vilikuwa kwa sehemu chuma na sehemu udongo wa mfinyanzi, hivyo ufalme huo kwa sehemu utakuwa na nguvu na kwa sehemu udhaifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vidole vya miguu yake nusu yao ni ya chuma nusu yao nyingine ni ya udongo, ni kwamba: Upande wa ufalme huo utakuwa wenye nguvu, lakini upande utakuwa unavunjikavunjika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama ulivyoona, vidole vyake vya miguu vilikuwa nusu chuma na nusu udongo wa mufinyanzi, na hii ina maana kwamba ufalme ule utakuwa na sehemu moja yenye nguvu na sehemu ingine yenye uzaifu.