Daniel 2:43 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hii inamaanisha kwamba watawala wa ufalme huo watachanganyikana kwa kuoana na watu wasio wa taifa lao, lakini hawatafaulu kuchanganyikana kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mfinyanzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama ulivyoona nyayo na vidole, sehemu moja vikiwa vya udongo uliochomwa na sehemu nyingine vya chuma, kadhalika ufalme huu utakuwa umegawanyika; wala hawatabaki wameungana tena, kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hii inamaanisha kwamba watawala wa ufalme huo watachanganyikana kwa kuoana na watu wasio wa taifa lao, lakini hawatafaulu kuchanganyikana kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mfinyanzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile ulivyoona chuma kikiwa kimechanganyikana na udongo wa mfinyanzi uliochomwa, ndivyo watu watakavyokuwa mchanganyiko wala hawatabaki kuwa wameungana tena kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mfinyanzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile ulivyoona chuma kikiwa kimechanganyikana na udongo wa mfinyanzi uliochomwa, ndivyo watu watakavyokuwa mchanganyiko, wala hawatabaki wameungana tena, kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mfinyanzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena umeona, chuma kilivyochanganyika na udongo wa mfinyanzi, ni kwamba: Wao watajichanganyachanganya na vizazi vya watu kwa kuoana, lakini hawataambatana mtu na mwenziwe, kama chuma kisivyochanganyikana na udongo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ina maana kwamba watawala wa ufalme huo watachanganyikana kwa kuoana na watu wasiokuwa wa taifa lao, lakini hawatafikia kuchanganyikana kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mufinyanzi.