Daniel 2:44 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wa wafalme hao, Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao kamwe hautaangamizwa. Watu wengine hawataushinda na kuutawala ufalme huo, bali ufalme huo utaziponda na kuzikomesha falme zilizotangulia, nao utadumu milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atauweka ufalme ambao kamwe hautaangamizwa, wala hautaachiwa taifa lingine. Utaziponda zile falme zote na kuzikomesha, bali wenyewe utadumu milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wa wafalme hao, Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao kamwe hautaangamizwa. Watu wengine hawataushinda na kuutawala ufalme huo, bali ufalme huo utaziponda na kuzikomesha falme zilizotangulia, nao utadumu milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atauweka ufalme ambao kamwe hautaangamizwa, wala hautaachiwa taifa jingine. Utaziponda zile falme zote na kuzikomesha, bali wenyewe utadumu milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atauweka ufalme ambao kamwe hautaangamizwa, wala hautaachiwa taifa jingine. Utaziponda zile falme zote na kuzikomesha, bali wenyewe utadumu milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile za wafalme hao Mungu wa mbinguni atatokeza ufalme usioangamika kale na kale, usiochukuliwa tena na kabila jingine, nao utauponda ufalme wote mwingine na kuutowesha, lakini wenyewe utakaa kale na kale,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa wafalme wale, Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao hautaangamizwa hata kidogo. Watu wengine hawataushinda na kuutawala ufalme huo, lakini ufalme huo utaziponda na kuzikomesha falme zilizotangulia, nao utadumu milele.