Daniel 2:46 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo mfalme Nebukadneza alipoanguka kifudifudi na kumsujudia Danieli na kuamuru wamtolee Danieli tambiko na ubani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mfalme Nebukadneza akaanguka kifudifudi mbele ya Danieli kumpa heshima, akaagiza wamtolee Danieli sadaka na uvumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo mfalme Nebukadneza alipoanguka kifudifudi na kumsujudia Danieli na kuamuru wamtolee Danieli tambiko na ubani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mfalme Nebukadneza akaanguka kifudifudi mbele ya Danieli kumpa heshima na kuagiza kwamba wamtolee Danieli sadaka na uvumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Mfalme Nebukadneza akaanguka kifudifudi mbele ya Danieli kumpa heshima, akaagiza wamtolee Danieli sadaka na uvumba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme Nebukadinesari alipoanguka kifudifudi, kisha akamwinamia Danieli, akaagiza kumtolea vipaji vya tambiko na uvumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mufalme Nebukadneza akaanguka uso mpaka chini na kumutukuza Danieli na kuamuru wamutolee Danieli sadaka na ubani.