Daniel 2:48 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme Nebukadneza akamtunukia Danieli heshima kubwa, akampa zawadi nyingi kubwakubwa, na kumfanya mtawala wa mkoa wote wa Babuloni, na mkuu wa wenye hekima wote wa Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo mfalme akamweka Danieli nafasi ya juu, na kumpa zawadi nyingi tele. Akamfanya mtawala wa jimbo lote la Babeli, na kumweka kuwa mkuu wa wenye hekima wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme Nebukadneza akamtunukia Danieli heshima kubwa, akampa zawadi nyingi kubwakubwa, na kumfanya mtawala wa mkoa wote wa Babuloni, na mkuu wa wenye hekima wote wa Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo mfalme akamweka Danieli kwenye nafasi ya juu na kumpa zawadi nyingi tele. Akamfanya kuwa mtawala wa jimbo lote la Babeli na kumweka kuwa mkuu wa wote wenye hekima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo mfalme akamweka Danieli nafasi ya juu, na kumpa zawadi nyingi tele. Akamfanya kuwa mtawala wa jimbo lote la Babeli, na kumweka kuwa mkuu wa wenye hekima wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme akampa Danieli macheo na matunzo mazuri mno, mengi sana, akampa nalo jimbo lote la Babeli, alitawale, awe mkuu wao watawala nchi wa kuwaamrisha wajuzi wote wa Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme Nebukadneza akamupandishia Danieli heshima kubwa, akamupa zawadi nyingi kubwakubwa, na kumufanya kuwa mutawala wa jimbo lote la Babeli, na mukubwa wa wenye hekima wote wa Babeli.