Daniel 2:49 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Danieli akamwomba mfalme, naye mfalme akawaweka Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa mambo ya utawala ya mkoa wa Babuloni. Lakini Danieli akabakia katika jumba la mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, kwa ombi la Danieli, mfalme akawateua Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa jimbo la Babeli, huku Danieli akibaki katika ukumbi wa mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danieli alikuwa akiketi katika lango la mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Danieli akamwomba mfalme, naye mfalme akawaweka Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa mambo ya utawala ya mkoa wa Babuloni. Lakini Danieli akabakia katika jumba la mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, kwa ombi la Danieli mfalme akawateua Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa jimbo la Babeli, huku Danieli akibaki katika ukumbi wa kifalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, kwa ombi la Danieli, mfalme akawateua Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa jimbo la Babeli, huku Danieli akibaki katika ukumbi wa mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Danieli alipomwomba mfalme, akawaagizia akina Sadiraki na Mesaki na Abedi-Nego kazi ya kuliangalia jimbo la Babeli, naye Danieli akakaa jumbani mwa mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danieli alikuwa akiketi katika lango la mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Danieli akamwomba mufalme, naye mufalme akawaweka Sadiraki, Mesaki na Abedenego kuwa wasimamizi wa mambo ya utawala ya jimbo la Babeli. Lakini Danieli akabakia katika nyumba ya mufalme.