Daniel 2:6 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mkiniambia hiyo ndoto na maana yake, nitawapa zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi, nijulisheni ndoto hiyo na maana yake!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mkiniambia ndoto yangu na kuifasiri, mtapokea kwangu zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto yangu na mnifasirie.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali kama mkinionyesha ile ndoto na tafsiri yake, nitawapa zawadi na thawabu na heshima nyingi; basi nionyesheni ile ndoto na tafsiri yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mkiniambia hiyo ndoto na maana yake, nitawapa zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi, nijulisheni ndoto hiyo na maana yake!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mkiniambia ndoto yangu na kuielezea, mtapokea kwangu zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto yangu na mnifasirie.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mkiniambia ndoto yangu na kuielezea, mtapokea kwangu zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto yangu na mnifasirie.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mkiweza kuieleza hiyo ndoto na maana yake, mtapata matunzo na vipaji na macheo makuu mbele yangu. Kwa hiyo ielezeni ndoto na maana yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali kama mkinionyesha ile ndoto na tafsiri yake, nitawapa zawadi na thawabu na heshima nyingi; basi nionyesheni ile ndoto na tafsiri yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mukiniambia hiyo ndoto na maana yake, nitawapa zawadi, mapato na heshima kubwa. Basi, munijulishe ndoto hiyo na maana yake!