Daniel 2:9 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kwamba msiponijulisha ndoto hiyo, adhabu yenu ni moja. Mmepatana kunidanganyadanganya na kunilaghailaghai huku muda unapita. Niambieni ndoto hiyo, nami nitajua kuwa mnaweza kunijulisha maana yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu, ipo adhabu moja tu kwenu. Mmepanga njama kuniambia habari za kunipotosha na mambo maovu, mkitumaini kwamba hali itabadilika. Hivyo basi, niambieni hiyo ndoto, nami nitajua kuwa mwaweza kunifasiria.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini msiponijulisha ile ndoto, iko amri moja tu iwapasayo; maana mmepatana kusema maneno ya uongo, na maneno maovu, mbele yangu, hata zamani zitakapobadilika; basi niambieni ile ndoto, nami nitajua ya kuwa mwaweza kunionyesha tafsiri yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwamba msiponijulisha ndoto hiyo, adhabu yenu ni moja. Mmepatana kunidanganyadanganya na kunilaghailaghai huku muda unapita. Niambieni ndoto hiyo, nami nitajua kuwa mnaweza kunijulisha maana yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu, ipo adhabu moja tu kwa ajili yenu. Mmefanya shauri kuniambia habari za kunipotosha na mambo maovu, mkitumaini kwamba hali itabadilika. Hivyo basi, niambieni hiyo ndoto, nami nitajua kuwa mwaweza kunifasiria.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu, ipo adhabu moja tu kwenu. Mmefanya shauri kuniambia habari za kunipotosha na mambo maovu, mkitumaini kwamba hali itabadilika. Hivyo basi, niambieni hiyo ndoto, nami nitajua kuwa mwaweza kunifasiria.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani msipoijulisha hiyo ndoto, amri, nitakayoitoa kwa ajili yenu, ni ile moja; kwani mmepatana kuniambia maneno ya uwongo na ya madanganyo, mpaka siku nyingine zitokee. Kwa hiyo niambieni ile ndoto, nijue, ya kuwa mtanieleza nayo maana yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini msiponijulisha ile ndoto, iko amri moja tu iwapasayo; maana mmepatana kusema maneno ya uongo, na maneno maovu, mbele yangu, hata zamani zitakapobadilika; basi niambieni ile ndoto, nami nitajua ya kuwa mwaweza kunionyesha tafsiri yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwamba musiponijulisha ndoto hiyo, azabu yenu ni moja. Mumepatana kunidanganyadanganya na kuniambia uongo kwa kungojea hali ibadilike. Muniambie ndoto hiyo, nami nitajua kwamba munaweza kunijulisha maana yake.