Daniel 3:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe, ee mfalme, ulitoa amri kuwa kila mtu anaposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na kila aina ya muziki, ainame chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee mfalme, umetoa amri kwamba kila mmoja atakayesikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari, na aina zote za sauti za ala za uimbaji, lazima asujudu na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe, ee mfalme, ulitoa amri kuwa kila mtu anaposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na kila aina ya muziki, ainame chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee mfalme, umetoa amri kwamba kila mmoja atakayesikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda, zumari na aina zote za ala za uimbaji lazima aanguke chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee mfalme, umetoa amri kwamba kila mmoja atakayesikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda, zumari na aina zote za ala za uimbaji lazima aanguke chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe mfalme umetoa amri kwamba: Kila mtu atakapozisikia sauti za mabaragumu na za filimbi na za marimba na za mapango na za mazeze na za mazomari na za namna zote za ngoma sharti aanguke na kukisujudia hicho kinyago cha dhahabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe, ee mufalme, ulitoa amri kwamba kila mutu anaposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zomari na kila aina ya muziki, ainame chini na kuiabudu ile sanamu ya zahabu.