Daniel 3:12 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, kuna Wayahudi fulani uliowateua kushughulikia mambo ya utawala wa mkoa wa Babuloni, yaani Shadraki, Meshaki na Abednego; watu hawa, ee mfalme, hawakuitii amri yako. Wanakataa kuitumikia miungu yako na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wako baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu ya mambo ya jimbo la Babeli, yaani Shadraki, Meshaki na Abednego, ambao hawakujali wewe, ee mfalme. Hawaitumikii miungu yako wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, kuna Wayahudi fulani uliowateua kushughulikia mambo ya utawala wa mkoa wa Babuloni, yaani Shadraki, Meshaki na Abednego; watu hawa, ee mfalme, hawakuitii amri yako. Wanakataa kuitumikia miungu yako na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wako baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu ya mambo ya jimbo la Babeli: yaani, Shadraki, Meshaki na Abednego, ambao hawakujali wewe, Ee mfalme. Hawaitumikii miungu yako wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wako baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu ya mambo ya jimbo la Babeli: yaani, Shadraki, Meshaki na Abednego, ambao hawakujali wewe, ee mfalme. Hawaitumikii miungu yako wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, wako waume wa Kiyuda, uliowaagizia kazi ya kuiangalia nchi ya Babeli, ndio Sadiraki na Mesaki na Abedi-Nego; waume hao hawakuishika amri yako, mfalme, wala hawaitumikii miungu yako, wala hawakiangukii hicho kinyago cha dhahabu, ulichokisimamisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, kuna Wayuda fulani uliowachagua kwa kushugulikia mambo ya utawala wa jimbo la Babeli, nao ni: Sadiraki, Mesaki na Abedenego; watu hawa, ee mufalme, hawakutii amri yako. Wanakataa kuitumikia miungu yako na kuiabudu ile sanamu ya zahabu uliyoisimamisha.