Daniel 3:15 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mtakaposikia tena sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na sauti za ala nyingine za muziki, je, mko tayari kuinama chini na kuiabudu sanamu niliyotengeneza? Kama mkikataa, mtatupwa mara moja katika tanuri ya moto mkali. Je, ni mungu gani anayeweza kuwaokoa mikononi mwangu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi wakati mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za ala za uimbaji, kama mtakuwa tayari kusujudu na kuiabudu hiyo sanamu niliyoitengeneza, vyema sana. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa saa hiyo hiyo ndani ya tanuru linalowaka moto. Naye ni mungu yupi ataweza kuwaokoa ninyi kutoka mkononi mwangu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mtakaposikia tena sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na sauti za ala nyingine za muziki, je, mko tayari kuinama chini na kuiabudu sanamu niliyotengeneza? Kama mkikataa, mtatupwa mara moja katika tanuri ya moto mkali. Je, ni mungu gani anayeweza kuwaokoa mikononi mwangu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wakati mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za ala za uimbaji, kama mtakuwa tayari kusujudu na kuiabudu hiyo sanamu niliyoitengeneza, vyema sana. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto. Naye ni mungu yupi atakayeweza kuwaokoa ninyi, kutoka katika mkono wangu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wakati mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za ala za uimbaji, kama mtakuwa tayari kusujudu na kuiabudu hiyo sanamu niliyoitengeneza, vyema sana. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto. Naye ni mungu yupi atakayeweza kuwaokoa ninyi, kutoka mkono wangu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama ninyi mko tayari siku, mtakapozisikia sauti za mabaragumu na za filimbi na za marimba na za mapango na za mazeze na za namna zote za ngoma, mwanguke na kukisujudia kila kinyago cha dhahabu, nilichokitengeneza, basi; lakini msipokiangukia, mtatupwa papo hapo ndani ya tanuru iwakayo moto. Tena yuko Mungu gani atakayewaokoa mkononi mwangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mutakaposikia tena sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zomari na sauti za ala nyingine za muziki, muko tayari kuinama chini na kuiabudu sanamu niliyotengeneza? Kama mukikataa, mutatupwa mara moja katika furu la moto mukali. Ni mungu gani anayeweza kuwaokoa katika mikono yangu?