Daniel 3:17 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa ndivyo, Mungu wetu ambaye tunamtumikia aweza kutuokoa katika tanuri ya moto mkali; tena atatuokoa mikononi mwako, ee mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa tutatupwa ndani ya tanuru linalowaka moto, Mungu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na moto, naye atatuokoa kutoka mkononi mwako, ee mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa ndivyo, Mungu wetu ambaye tunamtumikia aweza kutuokoa katika tanuri ya moto mkali; tena atatuokoa mikononi mwako, ee mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ikiwa tutatupwa ndani ya tanuru iwakayo moto, Mungu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na moto, naye atatuokoa kutoka mkononi mwako, Ee mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa tutatupwa ndani ya tanuru iwakayo moto, Mungu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na moto, naye atatuokoa kutoka mkononi mwako, ee mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, Mungu wetu, tunayemtumikia sisi, ndiye anayeweza kutuokoa katika tanuru iwakayo moto, namo mkononi mwako, mfalme, atatuokoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu wetu ambaye tunamutumikia anaweza kutuokoa. Atatuokoa kutoka furu la moto mukali na vilevile kutoka katika mikono yako, ee mufalme.