Daniel 3:19 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, mfalme Nebukadneza akawaka hasira, sura yake ikabadilika kwa chuki dhidi ya Shadraki, Meshaki na Abednego. Akaamuru mwako wa moto wa tanuri uongezwe mara saba kuliko kawaida yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Nebukadneza akawa na ghadhabu kali sana kwa Shadraki, Meshaki na Abednego, nayo nia yake ikabadilika kwao. Akaagiza tanuru lichochewe moto mara saba kuliko kawaida yake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, mfalme Nebukadneza akawaka hasira, sura yake ikabadilika kwa chuki dhidi ya Shadraki, Meshaki na Abednego. Akaamuru mwako wa moto wa tanuri uongezwe mara saba kuliko kawaida yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Nebukadneza akawa na ghadhabu kali sana kwa Shadraki, Meshaki na Abednego, nayo nia yake ikabadilika juu yao. Akaagiza tanuru ichochewe moto mara saba kuliko kawaida yake
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Nebukadneza akawa na ghadhabu kali sana kwa Shadraki, Meshaki na Abednego, nayo nia yake ikabadilika kwao. Akaagiza tanuru ichochewe moto mara saba kuliko kawaida yake
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, makali yenye moto yalipoushika moyo wote wa Nebukadinesari, nao uso wake ukawa mwingine kwa kuwaona akina Sadiraki na Mesaki na Abedi-Nego, akaagiza kabisa kuwasha moto mkubwa katika tanuru kuupita moto wake wa siku zote mara saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, mufalme Nebukadneza akawaka hasira, sura yake ikabadilika kwa chuki juu ya Sadiraki, Mesaki na Abedenego. Akaamuru kwamba moto wa furu uongezwe mara saba kuliko kawaida yake.