Daniel 3:2 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme akaamuru maliwali, wasimamizi, wakuu wa mikoa, washauri, watunza hazina, majaji, mahakimu na maofisa wote wa mikoa wahudhurie sherehe ya kuzindua rasmi sanamu aliyoisimamisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha mfalme akaita wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu, na maafisa wengine wote wa jimbo kuja kuizindua sanamu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme akaamuru maliwali, wasimamizi, wakuu wa mikoa, washauri, watunza hazina, majaji, mahakimu na maofisa wote wa mikoa wahudhurie sherehe ya kuzindua rasmi sanamu aliyoisimamisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha mfalme akaita wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wote wa jimbo kuja kuizindua sanamu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha mfalme akaita wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wote wa jimbo kuja kuizindua sanamu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme Nebukadinesari akatuma wajumbe, awakusanye wenye amri na wakuu na watawala nchi na waamuzi na watunza mali na mabwana shauri na wandewa na wakuu wote wa nchi, waje kukieua kinyago hicho, mfalme Nebukadinesari alichokisimamisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme akaamuru maliwali, wasimamizi, watawala, washauri, walinzi wa mali, waamuzi, wana sheria na wakubwa wote wa majimbo wahuzurie sikukuu ya kuzindua sanamu aliyosimamisha.