Daniel 3:23 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Shadraki, Meshaki na Abednego, wakiwa wamefungwa, wakatumbukia katika ile tanuri ya moto mkali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu hawa watatu walianguka ndani ya tanuru hilo la moto wakiwa wamefungwa kwa uthabiti sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Shadraki, Meshaki na Abednego, wakiwa wamefungwa, wakatumbukia katika ile tanuri ya moto mkali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu hawa watatu, wakiwa wamefungwa kwa uthabiti sana, walianguka ndani ya tanuru iwakayo moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu hawa watatu walianguka ndani ya tanuru iwakayo moto wakiwa wamefungwa kwa uthabiti sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wale waume watatu, Sadiraki na Mesaki na Abedi-Nego, wakaanguka ndani ya tanuru iwakayo moto wakiwa wamefungwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Sadiraki, Mesaki na Abedenego, wakiwa wamefungwa, wakatumbukia katika ile furu ya moto mukali.