Daniel 3:24 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mfalme Nebukadneza akashangaa, akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake, “Je, hatukuwafunga watu watatu na kuwatupa motoni?” Nao wakamjibu mfalme, “Naam, mfalme! Ndivyo!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mfalme Nebukadneza akashangaa, akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake, “Je, hawakuwa watu watatu ambao tuliwafunga na kuwatupa ndani ya moto?” Washauri wakajibu, “Hakika, ee mfalme.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mfalme Nebukadneza akashangaa, akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake, “Je, hatukuwafunga watu watatu na kuwatupa motoni?” Nao wakamjibu mfalme, “Naam, mfalme! Ndivyo!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mfalme Nebukadneza akashangaa akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake, “Je, hawakuwa watu watatu ambao tuliwafunga na kuwatupa ndani ya moto?” Washauri wakajibu, “Hakika, Ee mfalme.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Mfalme Nebukadneza akashangaa, akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake, “Je, hawakuwa watu watatu ambao tuliwafunga na kuwatupa ndani ya moto?” Washauri wakajibu, “Hakika, ee mfalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme Nebukadinesari akastuka, akainuka kwa upesi, akawaambia wasemaji wake wa shaurini kwamba: Je? Hatukutupa watu watatu ndani ya tanuru, nao walikuwa wamefungwa? Wakajibu, wakamwambia mfalme: Ndivyo kweli, mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mufalme Nebukadneza akashangaa, akasimama kwa haraka na kuwauliza washauri wake: Si tuliwafunga watu watatu na kuwatupa katika moto? Nao wakamujibu mufalme: Kweli, mufalme! Ndivyo!