Daniel 3:25 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akauliza, “Lakini sasa mbona ninaona watu wanne wakitembeatembea humo motoni bila kufungwa na wala hawadhuriki, na mtu wa nne anaonekana kama mwana wa miungu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akasema, “Tazama! Naona watu wanne wakitembeatembea ndani ya moto; hawajafungwa wala kudhurika, naye mtu yule wa nne anaonekana kama mwana wa miungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akauliza, “Lakini sasa mbona ninaona watu wanne wakitembeatembea humo motoni bila kufungwa na wala hawadhuriki, na mtu wa nne anaonekana kama mwana wa miungu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akasema, “Tazama! Naona watu wanne wakitembea-tembea ndani ya moto, hawakufungwa na hawakudhurika, naye mtu yule wanne anaonekana kama mwana wa miungu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akasema, “Tazama! Naona watu wanne wakitembeatembea ndani ya moto, hawajafungwa wala kudhurika, naye mtu yule wa nne anaonekana kama mwana wa miungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akajibu akisema: Tena inakuwaje? Mimi ninaona watu wanne wasiofungwa kabisa, wanatembea motoni, tena hawaungui hata kidogo; naye wa nne sura yake anafanana na mwana wa Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akauliza: Lakini sasa mbona ninaona watu wane wakitembeatembea mule ndani ya moto bila kufungwa na wala hawaunguwi, na mutu wa ine anaonekana kama mwana wa miungu?