Daniel 3:26 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mfalme Nebukadneza akaukaribia mlango wa tanuri ya moto mkali, akaita, “Shadraki, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Mkuu, tokeni mje hapa!” Shadraki, Meshaki na Abednego wakatoka motoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Nebukadneza akaukaribia mdomo wa lile tanuru lililowaka moto na kuita kwa sauti kuu, “Shadraki, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, tokeni! Njooni hapa!” Ndipo Shadraki, Meshaki na Abednego wakatoka ndani ya moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Nebukadreza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mfalme Nebukadneza akaukaribia mlango wa tanuri ya moto mkali, akaita, “Shadraki, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Mkuu, tokeni mje hapa!” Shadraki, Meshaki na Abednego wakatoka motoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Nebukadneza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iwakayo moto na kupaza sauti, “Shadraki, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, tokeni! Njoni huku!” Ndipo Shadraki, Meshaki na Abednego wakatoka ndani ya moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Nebukadneza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iwakayo moto na kupaza sauti, “Shadraki, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, tokeni! Njooni hapa!” Ndipo Shadraki, Meshaki na Abednego wakatoka ndani ya moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Nebukadinesari akalikaribia lango la tanuru iwakayo moto, akaita kwamba: Sadiraki na Mesaki na Abedi-Nego mnaomtumikia Mungu Alioko huko juu, tokeni nje! Ndipo, Sadiraki na Mesaki na Abedi-Nego walipotoka motoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Nebukadreza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mufalme Nebukadneza akaukaribia mulango wa furu la moto mukali, akaita: Sadiraki, Mesaki na Abedenego, watumishi wa Mungu Mukubwa, mutoke mukuje hapa! Sadiraki, Mesaki na Abedenego wakatoka ndani ya moto.