Daniel 3:27 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maliwali, wasimamizi, wakuu wa mikoa na washauri wa mfalme, wote wakakusanyika pamoja, wakaona ya kuwa ule moto haukuweza kuwaunguza hao watatu. Nywele zao hazikuungua, mavazi yao hayakuungua, wala hawakuwa na harufu yoyote ya moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao maliwali, wasimamizi, watawala na washauri wa mfalme wakakusanyika kuwazunguka. Waliona kwamba moto haukudhuru miili yao, wala unywele wa vichwa vyao haukuungua, majoho yao hayakuungua, wala hawakuwa na harufu ya moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na maamiri, na manaibu, na maliwali, na mawaziri, waliokuwa wamekusanyika pamoja, wakawaona watu hao, ya kuwa ule moto ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maliwali, wasimamizi, wakuu wa mikoa na washauri wa mfalme, wote wakakusanyika pamoja, wakaona ya kuwa ule moto haukuweza kuwaunguza hao watatu. Nywele zao hazikuungua, mavazi yao hayakuungua, wala hawakuwa na harufu yoyote ya moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao maliwali, wasimamizi, watawala na washauri wa kifalme wakakusanyika kuwazunguka. Waliona kwamba moto haukudhuru miili yao, wala unywele wa vichwa vyao haukuungua, majoho yao hayakuungua, wala hapakuwepo na harufu ya moto kwenye miili yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao maliwali, wasimamizi, watawala na washauri wa mfalme wakakusanyika kuwazunguka. Waliona kwamba moto haukudhuru miili yao, wala unywele wa vichwa vyao haukuungua, majoho yao hayakuungua, wala hapakuwepo na harufu ya moto kwenye miili yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wenye amri na wakuu na watawala nchi na wasemaji wa shaurini wa mfalme waliokuwa wamekusanyika hapo wakaona, ya kuwa moto haukuweza kuwafanyizia kitu watu hawa, nywele za vichwani pao hazikuungua, wala nguo zao hazikugeuka kuwa nyingine, wala mnuko tu wa moto haukuwapata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na maamiri, na manaibu, na maliwali, na mawaziri, waliokuwa wamekusanyika pamoja, wakawaona watu hao, ya kuwa ule moto ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maliwali, wasimamizi, wakubwa wa majimbo na washauri wa mufalme, wote wakakusanyika pamoja, wakaona kwamba ule moto haukuweza kuwaunguza hao watatu. Nywele zao hazikuungua, nguo zao hazikuungua wala hawakuwa na harufu yoyote ya moto.