Daniel 3:28 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mfalme Nebukadneza akasema, “Na asifiwe Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego kwa kuwa alimtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake ambao wanamtegemea. Wao walikataa kutii amri yangu ya kifalme, wakaitoa mhanga miili yao badala ya kuabudu mungu mwingine, ila Mungu wao peke yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Nebukadneza akasema, “Ahimidiwe Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego, ambaye amemtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake. Walimtumaini na kukaidi amri ya mfalme, nao wakawa tayari kufa kuliko kutumikia au kuabudu mungu mwingine yeyote isipokuwa Mungu wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mfalme Nebukadneza akasema, “Na asifiwe Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego kwa kuwa alimtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake ambao wanamtegemea. Wao walikataa kutii amri yangu ya kifalme, wakaitoa mhanga miili yao badala ya kuabudu mungu mwingine, ila Mungu wao peke yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Nebukadneza akasema, “Ahimidiwe Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego, ambaye amemtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake. Waliomtumaini na kutoogopa amri ya mfalme nao wakawa tayari kufa kuliko kutumikia au kuabudu mungu mwingine ye yote isipokuwa Mungu wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Nebukadneza akasema, “Ahimidiwe Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego, ambaye amemtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake. Walimtumaini na kukaidi amri ya mfalme, nao wakawa tayari kufa kuliko kutumikia au kuabudu mungu mwingine yeyote isipokuwa Mungu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nekukadinesari akasema kwamba: Na atukuzwe Mungu wao Sadiraki na Mesaki na Abedi-Nego, kwa kuwa amemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtegemea wakikataa kuifuata amri ya mfalme, wakaitoa miili yao, kwamba wasiangukie mungu wo wote na kuusujudia, ila Mungu wao tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mufalme Nebukadneza akasema: Asifiwe Mungu wa Sadiraki, Mesaki na Abedenego kwa sababu alimutuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake ambao wanamutegemea. Wao walikataa kutii amri yangu ya kifalme, wakaitoa miili yao kama sadaka pahali pa kuabudu mungu mwingine, lakini Mungu wao peke yake.