Daniel 3:5 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mkisikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na sauti za ala nyingine za muziki, lazima mwiname chini na kuiabudu sanamu ya dhahabu aliyosimamisha mfalme Nebukadneza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari, na aina zote za sauti za ala za uimbaji, lazima msujudu na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza ameisimamisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mkisikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na sauti za ala nyingine za muziki, lazima mwiname chini na kuiabudu sanamu ya dhahabu aliyosimamisha mfalme Nebukadneza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za sauti za ala za uimbaji, lazima mwanguke chini na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza ameisimamisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za sauti za ala za uimbaji, lazima mwanguke chini na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza ameisimamisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
siku, mtakapozisikia sauti za mabaragumu na za filimbi na za marimba na za mapango na za mazeze na za mazomari na za namna zote za ngoma, sharti mwanguke kukisujudia kinyago cha dhahabu, mfalme Nebukadinesari alichokisimamisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mukisikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zomari na sauti za ala nyingine za muziki, munapaswa kuinama chini na kuabudu sanamu ya zahabu mufalme Nebukadneza aliyosimamisha.