Daniel 4:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nilipokuwa nimelala, niliona maono haya: Niliona mti mrefu sana katikati ya dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya ndio maono niliyoona nilipokuwa nimelala kitandani mwangu: Nilitazama, na mbele yangu ulisimama mti katikati ya nchi. Ulikuwa mrefu sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; naliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nilipokuwa nimelala, niliona maono haya: Niliona mti mrefu sana katikati ya dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya ndiyo maono niliyoona nilipokuwa nimelala kitandani mwangu: Nilitazama, na mbele yangu ulisimama mti katikati ya nchi. Ulikuwa mrefu sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya ndiyo maono niliyoona nilipokuwa nimelala kitandani mwangu: Nilitazama, na mbele yangu ulisimama mti katikati ya nchi. Ulikuwa mrefu sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maono niliyoyaona kwa macho yangu, nilipolala kitandani, ni haya: nilikuwa nikitazama, mara nikaona mti katika nchi, uliokuwa mrefu sana kwa kimo chake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; naliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipokuwa ninalala katika kitanda, niliona maono: Mulinzi mutakatifu alishuka kutoka mbinguni.