Daniel 4:12 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Majani yake yalikuwa mazuri. Ulikuwa umejaa matunda, kiasi cha kuitosheleza dunia nzima. Wanyama wote wa porini walipata kivuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake. Viumbe vyote vilipata chakula kutoka mti huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Majani yake yalikuwa ya kupendeza, matunda yake yalikuwa mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Chini ya kivuli chake wanyama wa kondeni walipata hifadhi, na ndege wa angani waliishi katika matawi yake. Kila kiumbe kililishwa kutokana na mti huo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Majani yake yalikuwa mazuri. Ulikuwa umejaa matunda, kiasi cha kuitosheleza dunia nzima. Wanyama wote wa porini walipata kivuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake. Viumbe vyote vilipata chakula kutoka mti huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Majani yake yalikuwa ya kupendeza, matunda yake yalikuwa mengi, juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Chini ya kivuli chake wanyama wa kondeni walipata hifadhi na ndege wa angani waliishi katika matawi yake. Kila kiumbe kililishwa kutokana na mti huo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Majani yake yalikuwa ya kupendeza, matunda yake yalikuwa mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Chini ya kivuli chake wanyama wa kondeni walipata hifadhi, na ndege wa angani waliishi katika matawi yake. Kila kiumbe kililishwa kutokana na mti huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Majani yake yalikuwa mazuri, matunda yake yakawa mengi, vyakula vilivyopatikana kwake vikawatoshea watu wote pia, chini yake kivulini wakatua nyama wote wa porini, katika matawi yake ndege wa angani wakajenga viota vyao; hivyo wote wenye miili wakaushiba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini muache kisiki chake na mizizi yake ndani ya udongo, kwenye majani mabichi ndani ya shamba kikiwa kimefungwa pale kwa munyororo wa chuma na shaba. Muache kilowanishwe na umande wa mbinguni; muache kiishi pamoja na nyama wa pori na kula majani katika mbuga.