Daniel 4:14 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akapaaza sauti akisema, ‘Kateni mti huu na kuyakatakata matawi yake. Pukuteni majani yake na kuyatawanya matunda yake. Wanyama na watoroke chini yake na ndege kutoka matawi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaita kwa sauti kubwa: ‘Kateni mti huu, myafyeke matawi yake; yaondoeni majani yake na kuyatawanya matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake, na ndege waondoke kutoka matawi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akapaaza sauti akisema, ‘Kateni mti huu na kuyakatakata matawi yake. Pukuteni majani yake na kuyatawanya matunda yake. Wanyama na watoroke chini yake na ndege kutoka matawi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaita kwa sauti kubwa: ‘Kateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yaondoeni majani na kuyatawanya matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake na ndege wakimbie kutoka katika matawi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaita kwa sauti kubwa: ‘Kateni mti huu, myafyeke matawi yake; yaondoeni majani yake na kuyatawanya matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake na ndege waondoke kutoka matawi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaita kwa sauti ya nguvu kwamba: Ukateni mti huu! Yachanjeni matawi yake! Majani yake yapukuseni! Matunda yake yatapanyeni, nyama wakimbie chini yake, hata ndege waondoke katika matawi yake! Majani yake yapukuseni! Matunda yake yatapanyeni, nyama wakimbie chini yake, hata ndege waondoke katika matawi yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ni hukumu iliyotangazwa na walinzi; ni uamuzi wa wanaokuwa watakatifu, kusudi wanadamu wote kila pahali wapate kutambua kwamba Mungu Mukubwa ana mamlaka juu ya falme zote za wanadamu; yeye anamupatia ufalme mutu yeyote anayemupenda, anamufanya kuwa mufalme hata mutu muzaifu wa mwisho.