Daniel 4:15 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini acheni kisiki chake na mizizi yake ardhini, kwenye majani mabichi ya kondeni kikiwa kimefungwa hapo kwa mnyororo wa chuma na shaba. Mwacheni mtu huyo aloweshwe kwa umande wa mbinguni; mwacheni aishi pamoja na wanyama wa porini na kula nyasi mbugani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kiacheni kisiki na mizizi yake, kikiwa kimefungwa kwa chuma na shaba, kibaki ardhini, kwenye majani ya kondeni. “ ‘Mwacheni aloweshwe na umande wa mbinguni, naye aachwe aishi pamoja na wanyama miongoni mwa mimea ya dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini acheni kisiki chake na mizizi yake ardhini, kwenye majani mabichi ya kondeni kikiwa kimefungwa hapo kwa mnyororo wa chuma na shaba. Mwacheni mtu huyo aloweshwe kwa umande wa mbinguni; mwacheni aishi pamoja na wanyama wa porini na kula nyasi mbugani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini acheni kisiki chake na mizizi, kikiwa kimefungwa kwa chuma na shaba, kibaki ardhini, kwenye majani ya kondeni. “ ‘Mwacheni aloweshwe na umande wa mbinguni, naye aachwe aishi pamoja na wanyama miongoni mwa mimea ya dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini acheni kisiki chake na mizizi, kikiwa kimefungwa kwa chuma na shaba, kibaki ardhini, kwenye majani ya kondeni. “ ‘Mwacheni aloweshwe na umande wa mbinguni, naye aachwe aishi pamoja na wanyama miongoni mwa mimea ya dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini shina lenye mizizi yake liacheni mchangani, likiwa limefungwa kwa vyuma na kwa shaba katika mbuga yenye majani mabichi, liloweshwe na umande wa mbinguni, yale majani ya nchi yawe fungu lake, nalo lao nyama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ndiyo ndoto niliyoota mimi Nebukadneza. Sasa, wewe Beltesaza, unielezee maana yake; maana wenye hekima wote katika ufalme wangu hawawezi kuniambia maana yake; lakini wewe utaweza kwa maana roho ya miungu mitakatifu iko ndani yako.