Daniel 4:18 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hii ndiyo ndoto niliyoota mimi Nebukadneza. Sasa, wewe Belteshaza, nieleze maana yake; kwani wenye hekima wote katika ufalme wangu hawawezi kuniambia maana yake; lakini wewe utaweza kwa kuwa roho ya miungu mitakatifu imo ndani yako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hii ndiyo ndoto niliyoipata mimi, Mfalme Nebukadneza. Sasa Belteshaza, niambie maana yake, kwa maana hakuna hata mmoja wa wenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunifasiria. Bali wewe unaweza, kwa sababu roho ya miungu mitakatifu iko ndani yako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi, Nebukadreza, nimeiona ndoto hii; na wewe, Ee Belteshaza, eleza tafsiri yake, kwa maana wenye hekima wote wa ufalme wangu hawawezi kunijulisha tafsiri yake; bali wewe waweza, maana roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hii ndiyo ndoto niliyoota mimi Nebukadneza. Sasa, wewe Belteshaza, nieleze maana yake; kwani wenye hekima wote katika ufalme wangu hawawezi kuniambia maana yake; lakini wewe utaweza kwa kuwa roho ya miungu mitakatifu imo ndani yako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hii ndiyo niliyopata mimi, Mfalme Nebukadneza. Sasa Belteshaza, niambie maana yake, kwa maana hakuna hata mmoja wa wenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunifasiria. Bali wewe waweza, kwa sababu Roho ya Miungu Mitakatifu imo ndani yako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hii ndiyo ndoto niliyoipata mimi, Mfalme Nebukadneza. Sasa Belteshaza, niambie maana yake, kwa maana hakuna hata mmoja wa wenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunifasiria. Bali wewe waweza, kwa sababu roho ya miungu mitakatifu imo ndani yako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndoto hii nimeiota mimi mfalme Nebukadinesari, nawe Beltesasari iseme maana yake, kwa kuwa wajuzi wote wa ufalme wangu hawakuweza kunijulisha maana yake lakini wewe utaweza, kwani roho ya miungu mitakatifu imo mwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi, Nebukadreza, nimeiona ndoto hii; na wewe, Ee Belteshaza, eleza tafsiri yake, kwa maana wenye hekima wote wa ufalme wangu hawawezi kunijulisha tafsiri yake; bali wewe waweza, maana roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
majani yake yakiwa mazuri, na matunda yake mengi ya kukulisha viumbe vyote, nyama wa pori wakipata kivuli chini yake, na ndege wakikaa katika matawi yake,