Daniel 4:19 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Danieli, aliyeitwa pia Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akamwambia, “Belteshaza, ndoto hii, wala maana yake visikufadhaishe!” Belteshaza akamjibu, “Bwana wangu, laiti ndoto hii na maana yake ingewahusu adui zako!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza) alipofadhaika sana kwa muda, nayo mawazo yake yakamtia hofu. Basi mfalme akasema, “Belteshaza, usiruhusu ndoto wala maana yake kukutia hofu.” Belteshaza akajibu, “Bwana wangu, laiti ndoto hii ingewahusu adui zako, na maana yake iwahusu watesi wako!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Danieli, aliyeitwa pia Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akamwambia, “Belteshaza, ndoto hii, wala maana yake visikufadhaishe!” Belteshaza akamjibu, “Bwana wangu, laiti ndoto hii na maana yake ingewahusu adui zako!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza) alipofadhaika sana kwa kitambo, nayo mawazo yake yakamtia hofu. Basi mfalme akasema, “Belteshaza, usiruhusu ndoto wala maana yake kukutia hofu.” Belteshaza akamjibu, “Bwana wangu, laiti ndoto hii ingehusu adui zako na maana yake iwahusu watesi wako!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza) alipofadhaika sana kwa muda, nayo mawazo yake yakamtia hofu. Basi mfalme akasema, “Belteshaza, usiruhusu ndoto wala maana yake kukutia hofu.” Belteshaza akamjibu, “Bwana wangu, laiti ndoto hii ingehusu adui zako, na maana yake iwahusu watesi wako!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Danieli aliyeitwa jina lake Beltesasari akapigwa bumbuazi kitambo kidogo, mawazo yake yakamstusha; ndipo, mfalme alipomwambia Beltesasari kwamba: Ndoto na maana yake isikustushe! Beltesasari akamjibu akasema: Bwana wangu, ningependa, ndoto hii iwe yao wakuchukiao, nayo maana yake iwapate wakuinukiao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
basi, ni wewe, ee mufalme, ambaye umekuwa mukubwa na mwenye nguvu. Ukubwa wako umefika mpaka mbinguni, na ufalme wako umeenea mpaka miisho ya dunia.